Baada ya mshambuliaji wa kimataifa wa Sweden Zlatan Ibrahimovic kutangaza kuihama Man United na kujiunga na club ya LA Galaxy ya Marekani, wengi wanaamini kuwa Zlatan ameondoka Man United baada ya kuwa na majeraha.

Ukweli umetolewa leo Dr  Freddie Fu Ho-Kueng aliyekuwa anamtibia Zlatan Ibrahimovic kuwa ameondoka Man United kufuatia Man United kutolewa katika michuano na UEFA Champions League, mashindano ambayo hajawahi kutwaa taji hilo licha ya kuvichezea vilabu vya Barcelona, Inter Milan na AC Milan.

Zlatan alianza kupoteza namba Man United baada ya kupata jeraha la goti katika msimu wa 2016/2017, hivyo baada ya kuongeza mkataba wake na kurudi mwezi November alimudu kuichezea Man United katika mechi tano tu za Ligi hivyo wakaamua kuvunja mkataba na Man United kwa makubaliano ya pande zote mbili.

Dr Freddie Fu Ho-Kueng ameeleza kuwa Zlatan Ibrahimovic alikuwa na ndoto ya kutwaa taji la UEFA Champions League akiwa na Man United na kutimiza ndoto yake ya kutwaa taji hilo ambalo amekuwa akilikosa kwa muda mrefu, hivyo baada ya Man United kutolewa ndio akaamua kwenda kucheza Marekani.