Teknolojia ya robot inazidi kupamba moto katika maeneo mbalimbali duniani huku wataalamu wengi wakiamini kuwa kwa miaka ijayo ndio teknolojia itakayochukua nafasi kubwa katika maeneo mengi ya utendaji.

Kutoka nchini Japan wameanza kutumika katika kituo cha kutunza wazee Jijini Tokyokijulikanacho kama Tokyo’s Shin-tomi nursing home ambacho kwasasa kinatumia aina takribani 20 za robot ili kuwahudumia wazee hao.

Serikali ya Japan imeeleza kuwa inatumaini teknolojia hii itakuwa mfano wa ujuzi wa kusaidia wazee na kuwalea katika siku za mbeleni.