Uamuzi wa serikali ya Uganda kuanzisha ada ya majaribio ya hiari kwa Covid-19 inaweza kupelekea kuvuruga safari na kuanza tena kwa utalii, na pia biashara.

Aidha uamuzi huo unaweza kuathiri hata kurudi kwa raia wa Uganda kutoka nje.

Siku ya Jumapili jioni, serikali ilitoa agizo linalohitaji wakala kulipisha $ 65 (£ 50) kwa kila jaribio la Covid 19 ambapo hali hiyo inaathiri madereva wa malori ya kuvuka mpaka, wageni nchini humo na Waganda wanaokwenda nyumbani.

Mashirika ambayo yanapanga kupima wafanyikazi wao na watu binafsi, ambao wanataka kujua ikiwa wameambukizwa virusi, watalazimika pia kulipa ada hiyo.

Serikali huko Kampala inasema ada hiyo itachangia gharama za kudhibiti janga hilo. Kufikia sasa, watu 350,000 wamejaribiwa, kukiwa na visa 2,900 na vifo 30.

Facebook Comments