Baada ya kunusurika na kushuka daraja kwa msimu ulioisha wa mwaka 2019/20, sasa kuelekea msimu huu Mtibwa Sugar wameonesha kujifunza na hawatakubali tena kurudia kosa hilo msimu huu.


Klabu hiyo ya yenye maskani yake Mjini Morogoro huko Turiani kupitia Afisa Habari wake ndugu Thobiasi Kifaru, wamejinasibu kuwa wamejifunza mengi kutokana na makosa ya msimu ulioisha na sasa msimu huu amewaahidi Wana Mtibwa na wapenzi wote wa Manungu Turiani kuwa Watabeba Ubingwa wa Ligi Tanzania Bara au kama sio Ubingwa basi watamaliza katika nafasi tatu bora za juu ya msimamo wa Ligi ya msimu wa 2020/2021.


Kifaru aliyasema hayo alipokuwa akihojiwa na Mtayarishaji wa kipindi cha Chandimu cha hapa Times fm kinachoruka kila siku asubuhi ya saa 3 hadi saa 4 kamili.

Facebook Comments