Msanii kutoka katika kiwanda cha bongo flava Judith Wambura Mbibo (Lady Jaydee) ambae amekuwa na mchango mkubwa katika kuliendeleza soko la muziki nchini na nje ya mipaka jana amepiga story na Times Fm digital na kuzungumzia ujio wa Tamasha lake na kusherehekea miaka Ishirini katika Muziki wa bongo Flava.

      Aidha Mwanadada uyo ambae anatikisa katika vibao mbali mbali vya Muziki wa bongo flava amesema kuwa katika Tamasha lake asingeweza kualika wasanii wote kwa kuwa wasanii aliowaalika wanatosha.

      Jidee amesema kuwa katika nyimbo zake aliamua kumshirikisha Maunda Zolo kwani maundo ni mdogo wake na amekua akimshirikisha kwenye mambo ya muziki hata hivyo amesema kuwa alihitaji sauti ya maundo kuwepo kwenye kibao chake.
      
       “Nyimbo zangu zote nazipenda ila nimeamua kuchagua nyimbo wanazozipenda watu ndio nitaimba hata hivyo watu wamekua wakitengeneza maneno ila mimi huwa namuongelea vizuri Khadija kopa na Zuchu atakuepo akimuwakilisha mama yake”

        Lady Jaydee amepiga stori na kusema kuwa awezi kufanya Record Label na kudai kuwa wanamuziki wanaweza kupitia kwenye mikono yake lakini sio Record label na kuomba watu wafike kwa wingi kwenye Tamasha lake.

Facebook Comments