Chuo kikuu cha Namibia kupitia kitengo chake cha wanyama, kinafunza Mbwa kuweza kumtambua wagonjwa wa COVID-19. Mfunzo hayo yanayondeshwa na Madaktari wazoefu Wanyama na wafugaji na watunzaji wazoefu wa Mbwa.


Mbwa aina ya German Shephard wana uwezo mkubwa wa kunusa harufu ya tofauti inayotoka kwa mginjwa wa COVID-19.


Mpango ni kuweka Mbwa kwenye Viwanja vya Ndege na mipakani alisema Daktari Conrad Brain ambae ni Mwalimu wa physiology na epidemiology. Daktari wa wanyama na Mwalimu Alma Raath pia amesema, Mbwa wamekuwa na uwezo wa kutambua wagonjwa wenye Virusi vya Korona kiusahihi kwa 95% .
Mafunzo hayo yalianza miezi miwili iliyopita, lakini haijasemwa ni lini yatakamilika. Gazeti la “The Namibian” limesema hii ni nchi ya kwanza Afrika kutumia Mbwa kwa ajili ya kutambua wagonjwa wa COVID-19. Nchi nyingine zinazotumia mnyama huyu kutambua wagonjwa hao ni United Arab Emirates (UAE), Chile, Ajentina, Brazil and Ubelgiji.

Facebook Comments