Rapper Kanye West aliyekuwa na ndoto ya kuwa rapper wa kwanza kuliongoza taifa la Marekani, ameshuhudia ndoto yake hiyo ikiota mbawa kila kukicha. Hii ni baada ya mahakama ya mji wa Wisconsin kutoa hukumu yake kuwa Kanye alichelewa kurejesha fomu hivyo hapaswi kuwekwa kwenye karatasi ya kupigia kura jimboni hapo.

Rapper Kanye West


Wiki mbili zilizopita Kanye alipaswa kurejesha fomu za kuthibitisha nia ya kugombea uraisi katika mji huo wa Wisconsin. Zoezi hilo lilipaswa kufikia ukomo saa 5 asubuhi na Kanye alifika ofisini akiwa amechelewa dakika chache tu lakini wahusika walikataa kupokea fomu zake na kufunga milango ya ofisi. Hivyo ilimlazimu Kanye aende mahakamani kusaka haki zaidi.


Katika hukumu ya kesi hiyo jaji alisema kuwa mgombea yeyote hasa wa uraisi anapaswa kuwa anajua tofauti ya saa 5 kamili na saa 5 na dakika 1. Akasema kuwa kama Kanye alifika baada ya muda uliopangwa basi si tu hapaswi bali pia hafai kuwemo kwenye karatasi ya mpiga kura.
Mpaka sasa Kanye ameondolewa kwenye karatasi ya mpiga kura katika majimbo zaidi ya 10 ikiwemo jimbo la nyumbani kwao Illinos.

Facebook Comments