Mamlaka ya udhibiti wa nishati na maji EWURA mkoani Mbeya imewataka watumiaji wa nishati ya mafuta hususani petrol kufuata sheria na taratibu zilizowekwa na mamlaka hiyo pindi wanapoenda katika vituo vya kuuza mafuta.


Wito huo umetolewa na Mhandisi RAPHAEL NYAMAMU ambaye ni mkaguzi mwandamizi wa nishati ya mafuta kwa nyanda za juu kusini ambapo amesema katika kila kituo cha mafuta EWURA imebandika matangazo yanayoonesha vitu ambavyo mteja anapaswa kuvifuata
NYAMAMU amewataka madereva wenye tabia ya kwenda katika vituo vya mafuta wakiwa na abiria ndani ya gari kuacha mara moja ili kulinda usalama wa abiria wao


Mmoja wa wafanyakazi katika kituo cha kujaza mafuta ameeleza kuwa licha ya uwepo wa sheria hizo lakini bado kumekuwa na changamoto kwa baadhi ya madereva kukaidi ikiwemo suala la kuzima simu Baadhi ya madereva  wamekiri kuwa miongoni mwao hawafuati sheria hizo huku wakiwatupia lawana madereva ambao hawajapata mafunzo kutoka VETA.


Hata hivyo wameiomba mamlaka husika kuendelea kutoa elimu kwa madereva wote ikiwa ni kwa lengo la kukumbushana kufuata sheria hizo.

Facebook Comments