Tanzania na Uganda zimesaini mkataba wa makubaliano ya ujenzi wa bomba la mafuta la urefu wa 1,445 km (898 miles). Bomba hilo litakalo toka Uganda mpaka mpaka bandari ya Tanga litagharimu kiasi cha $3.5bn (£2.7m).

Rais Magufuli akiwa na Rais Museven


Kampuni ya TOTAL ya Ufaransa na Wachina wa CNOOC, ndio zinafanya kazi bega kwa bega na Serikali za Uganda and Tanzania. Sherehe za kusaini makubaliano hayo zilizo hudhuriwa na Marais wa Nchi zote mbili.


Uganda iligundua kuwa na Mafuta mwaka 2006 lakini mchakato wa uzalishaji ulichelewa kutokana na uhaba wa miundo mbinu ikiwemo Bomba la usafirishaji.


Tarehe ya kuanza ujenzi wa Bomba hilo ambalo litakalokuwa kubwa kuliko yote Africa Mashariki bado haija tangazwa.


Repoti moja ya Federation for Human Rights (FIDH) inasema zaidi ya Famili 12,000 za huko nchini Uganda zitaathirika na ujenzi au upitishaji wa Bomba hili kwa kuhamishwa makazi. Pia repoti imesema hata baadhi ya sehemu za uoto wa asili zitaathirika.


80% ya Bomba lote litakuwa linapita Tanzania na kutengeneza ajira zaidi ya 18,000 kwa Watanzania.

Facebook Comments