Weekend hii African Music Magazine wameachia list ya majina ya wasanii watakaoshiriki kuwania tuzo za Afrimma katika vipengele tofauti mwaka huu. Katika list hiyo bado majina makongwe kama Burna Boy, Diamond Platnumz, Davido, Master KG nk yameendelea kuwepo na majina mapya kama Oxlade, Zeynab,Zuchu na engine yakitia maguu kwa mara ya kwanza.


Wasanii wa Tanzania waliong’aa kwenye list hiyo ni pamoja na Diamond Platnumz aliyetajwa katika vipengele vitano tofauti, vikiwemo vya msanii wa mwaka na wimbo wa mwaka, Harmonize kipengere kimoja, Ali Kiba vipengele viwili, Mbosso (2), Zuchu (2) Rayvany(1), Maua Sama(1) Nandy(1) Navy Kenzo (1) Rosa Ree (2) na Director Kenny (1).

Rapper Rosa Ree


Burna boy kutoka Nigeria ndiye anayeongoza kwa kutajwa mara nyingi zaidi katika vipengele 7 akifuatiwa na Dimond Platnumz aliyetajwa mara 5 huku Zuchu akiwakilisha katika tuzo ya msanii mpya na Rosa Ree akiwa rapper pekee kutoka bongo kwenye list hiyo.


Kutokana na janga la Corona kuendelea kuitesa dunia, Waandaaji wa tuzo hizo wamesema shughuli ya ugawaji itafanyika kimtandao na watu watashuhudia perfoance kali kutoka kila kona ya dunia kupitia runinga zao. Tuzo hizo zinatarajiwa kugawiwa tarehe 15 November ikiwa ni msimu wake wa 7.


Story By: Clement Mbudu

Zege2020

Facebook Comments