Wakimbizi sita kutoka Sudan ya Kusini wameuwawa na wengine wanne kujeruhiwa katika kambi ya Madi Okollo, Kaskazini Mashariki mwa Uganda. Msemaji wa Polisi Josephine Angucia, amesema Polisi inawashikilia wanakijiji 13 wanaoshukiwa kwa mauaji hayo waliyotokea Ijumaa.


Mauwaji hayo yalianza baada kundi moja la wakimbizi kumpiga kijana wa maeneo hayo,Bw. Ajute Rahman Yassin, aliyekuwa akilisha wanyama wake karibu na kambi hiyo. Kulikuwa na uvumi Bw. Ajute alifairiki Dunia kitendo kilichozua mfarakano huo na shambulio kwenye kambi hiyo.
Jeshi la la polisi bado linawasaka washukiwa wengine.


Uganda ni nchi yenye wakimbizi wengi kuliko nchi nyingine zote Afrika, Uganda in wakaimbizi wapatao 1.4 mil. Wengi wa wakimbizi hao wakitokea Sudan ya Kusini. katika Miaka ya hivi karibu kumekuwa na vuguvugu kutoelewana kati ya wakimbizi na wenyeji juu ya Ardhi, Kuni na Maji.


Ripoti kutoka kwa umoja wa Haki za Wakimbizi wa Kimataifa(International Refugee Rights Initiative) ya mwaka wa jana ulisema kungeweza kutokea vurugu kati ya majirani hao.

Facebook Comments