Ni mwezi sasa umepita tangu taarifa za muimbaji mkongwe kutoka Marekani R. Kelly kushambuliwa jela na mfungwa mwenzie katika kituo cha Metropolitan Correctional Center.

Leo katika mahojiano rasmi na Chicago Sun Times, moja ya mawakili wa Kells, Nicole Blank Becker amefunguka kuwa kwa sasa muimbaji huyo amekuwa akiishi kwa hofu na muda mwingine kugoma kutoka kwenye chumba chake hata muda ambao hupewa ruhusa ya kufanya hivyo.  

Hiyo inaelezwa kusababishwa na shambulio alilolipata mwezi uliopita kutoka kwa Jeremiah Shane Farmer mfungwa mwenzie, jambo ambalo limemfanya R Kelly kuhofia usalama wa maisha yake.

Iliripotiwa kuwa Jeremiah alimshambulia Kellz kwa kumpiga kichwani, kifuani pamoja na kujaribu kumchoma na peni. Baada ya tukio hilo ilielezwa kuwa Jeremiah alihamishiwa katika kituo kingine mjini Michigan baada ya kuthibitisha mwenyewe kuwa alifanya tukio hilo.

Mawakili wa R.Kelly wamekuwa wakipambana kuhakikisha mteja wao anaachiwa kwa njia mbalimbali ikiwemo ile ya kudai kuwa kutokana na umri wa Kellz unamuweka kwenye kundi ambalo liko hatarini kupata COVID-19, japo ombi hilo lilikataliwa.

Facebook Comments