Wako wapi akina Juan Sebastian Veron akitokea Lazio,wapi Diego Forlan,vipi unamkumbukua Gabriel Heinzie wewe!? Bila kumsahau  Anderson fundi wa mguu wa kushoto. Je, vipi kuhusu Carlos Tevez na wale mapacha akina Rafael da silva na ndugu yake Fabio

Hivi karibuni Sergio Romero, Antonio Valencia, Marcos Rojo “Chuma” Andreas Pereira na Radamel Falcao ni baadhi ya nyota kutoka bara la Amerika ya kusini walio wahi na walipo pale Old Trafford, sehemu ambayo ndio chumba cha vikombe,Lakini wameshindwa kudumu au kujihakikishia namba katika timu hiyo.

Ulimwengu wa Soka unajiuliza tatizo ni nini hasa, linalofanya wachezaji ambao baadhi yao ni bora kabisa duniani, lakini wameshindwa kufanya vizuri na kudumu ndani ya Manchester United.  Je, Tatizo ni utamaduni, uwezo wa hawa Wachezaji,au ni nini hasa?

Manchester Unites sasa  imemsajili Edison Roberto Canani(33) mzaliwa wa Salto, Kaskazini Magharibi mwa Uruguay. Pamoja na Alex Telles(27) Mbrazil mwenye Uraia wa Italy. Swali kichwani mwa washabiki wengi ni je, Wamarekani wa Kusini hawa watakuwa na tofauti hapa Old Trafford na wenzao waliopita au safari hii itakuwa tofauti.

Je Cavani na Telles wanaingia moja kwa moja kwenye 11 ya kuanza au Sabu? Je, Cavani atafanikiwa United kuliko Ibrahimovic United? Telles na Shaw nani ataanza? Majibu ya yote haya tutayapata kadri ya muda unavyo kwenda.

Facebook Comments