Wakali wa muziki wa taarabu nchini Khadija Omari Kopa na Isha Ramadhani wamesema kwasasa wapo ‘likizo’ baada ya kubanwa na kampeni za Uchaguzi Mkuu zinazoendelea nchini nzima.

Wakipiga stori na Mwandishi Wetu wasanii hao wenye heshima kubwa katika muziki huo walisema kwasasa wamesimamisha shughuli zote za burudani na wamejikita katika kampeni za uchaguzi ambazo ukomo wake ni Octoba 28 mwaka huu.

Isha Mashauzi

“Unajua kila kitu kinawakati wake kulikuwa na wakati wa burudani na sasa ni wakati wa kampeni kupata viongozi ambao watatuongoza kwa miaka 5. Kipindi hiki ni kipindi cha kuwanadi na kusikilize sera za wagombea sasa ukifanya maonyesho utawapa wapi muda wa kuwanadi na kuwasikiliza wagombea? Ni ngumu ndio maana nimeweka kando masuala ua burudani na nimejikita na uchaguzi Mkuu,” alisema Hadija Kopa.

Alisema kuimba ndio kazi inayomuweka mjini hivyo anaiheshimu sana.

“Mashabiki wanivumilie tu kwasasa unajua uchaguzi unakuja mara moja kila baada ya miaka mitano baada ya hapo burudani zitaendelea kwasababu hii ndio kazi yangu siwezi kuiacha,” alisema.

Kwa upande wa Isha Ramadhani alisema amekuwa akipokea simu nyingi toka kwa mashabiki zake pamoja na wadau wa muziki wa taarabu lakini amekuwa akishindwa kutimiza matakwa yao kutokana na kubanwa na uchaguzi mkuu.

“Najua amashabiki wamemiss sana burudani zangu lakini wavumilie tarehe 28 wala sio mbali baada tu ya uchaguzi burudani zitaendelea kwa sasa nipo likizo fupi ya uchaguzi,” alisema Isha.

Facebook Comments