Msanii mwenye mbwembwe na ‘vurugu’ za kiwango cha juu katika kulishambulia jukwaa, Abubakar Suddy ‘Prince Amigo anakuja na bonge moja la ‘party’ katika kufurahia miaka 17 ya kutoa burudani.

Amigo ambaye kwasasa ni Mkurugenzi wa benfi ya First Class Modern Taarab amesema kwasasa yupo katika maandalizi ya mwisho katika kuhakikisha siku hiyo mashabiki wanapata ile kitu roho inataka.

“Tupo kwenye maandalizi ndugu yangu kama unavyojua kuwepo kwenye tasnia kwa miaka 17 si kitu kidogo kwa hiyo hata hiyo shughuli inabidi iwe ya kiwango cha juu sana ‘so’ tupo kwenye maandalizi ya mwisho kabla ya kutoa burudani pale Lekam Hotel Bugurini,” alisema Amigo.

Alisema ili kuifanya siku hiyo kuwa ya kipekee kutakuwa na wasanii pamoja na bendi nyingine za taarabu pamoja na wasanii wa miduara ili kuhakikisha mashabiki wanasherehekea vyema miaka 17 ya uwepo kwenye kwenye muziki wa taarab.

Facebook Comments