Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu, hatimaye bendi ya kitambo ya muziki wa taarabu nchini Naksh Naksh Modern Taraab ‘Bendi ya Wananchi’ imerejea kwa kishindo.

Mkurugenzi wa bendi hiyo Faza Mauji aliiambia times fm wiki iliyopita kuwa kwasasa bendi hiyo imedhamiria kurudisha makali yake baada ya kitikiswa kiuchumi kutokana na tatizo la Corona.

“Unajua corona ilituharibia sana hasa baada ya shughuli zote za sanaa kusimamishwa na serikali. Lakini baada ya tatizo kuisha na mambo kuwa safi tunataka kuwaonyesha mashabiki wetu kwamba bendi ipo nab ado makali yake yapo palepale,” alisema Faza.

Amesema kipindi chote ambacho shughuli za muziki zilisimamishwa na serikali waliutumia muda huo kutengeneza nyimbo za bendi ambazo sasa wanazitambulisha kwa mashabiki zao.

“Kwasasa tumeanza kuutambulisha wimbo wetu mpya uitwao ‘Waja Mnanongwa’ ulioimbwa na Farida Kitamba baada ya huu kwenda kwa wiki tatu hadi nne tutaachia wimbo wa pili.”

Facebook Comments