‘Tuor’ ya ‘Narudi Mjini’ ya msanii wa kiwango cha juu katika muziki wa taarab nchini Mzee Yusuf nimezidi kushika kasi baada ya sasa tuor hiyo kuhamia mikoani.

Taarifa toka ndani ya bendi ya Jahazi Modern Taarab imesema msanii huyo baada ya kufanya ziara katika viunga mbalimbali vya jijini la Dar kwasasa ameanza masafa marefu ya kwenda mikoni.

“Kama tulivyosema awali kwamba baada ya Mzee kurejea rasmi kwenye muziki wa taarab, tunataka kumfikia kila shabiki yetu ili kila aliyemiss birudani zetu aweze kuzipata,” alisema Hamisi Hassan ‘Boha’ Meneja wa Mzee Yusuf.

Katika taarifa yake kwa mwandishi wetu, Boha amesema wiki iliyopita Jahazi walikuwa mkoani Geita katika ukumbi wa Ambassador ambapo mbali ya kutoa burudani kwa mashabiki zao pia walitembea watoto wanaoishi katika mazingira magumu.

Bendi hiyo wiki hii itaendelea na ziara zake katika mikoa ya Shinyanga, Tabora, Singida na Manyara.

Facebook Comments