Kansela Angela Merkel na viongozi wakuu wa majimbo 16 ya Ujerumani wamekubaliana kuongeza makali kwa amri ya kuvaa barakoa pamoja na kuamuru kufungwa mapema kwa maduka ya kuuza pombe katika maeneo yenye kiwango cha juu cha maambukizi ya virusi vya corona.

Makubaliano hayo yamefikiwa baada ya mkutano uliofanyika jana saa chache baada ya Ujerumani kuporipoti maambukizi mapya 5,000 ya virusi vya corona katika kipindi cha saa 24, kiwango ambacho ni kikubwa kuwahi kushuhudiwa tangu katikati ya mwezi April.

Mapendekezo yaliyotolewa yanataka amri ya kuvaa barakoa ambayo tayari ni lazima ndani ya vyombo vya usafiri na maduka nchini Ujerumani itekelezwe pia kwenye maeneo ya umma yaliyo na msongamnao katika wilaya zenye maambukizi makubwa ya COVID-19.

Miji mingi ya Ujerumani ikiwemo, Berlin, Cologne, Duesseldorf, Frankfurt na Munich imeshuhudia wimbi jipya la maambukizi ya virusi vya corona hatua iliyolazimisha kurejeshwa kwa vizuizi vya kuzuia kusambaa virusi hivyo.

Facebook Comments