Polisi nchini Thailand  imewatawanya waandamanaji waliopiga kambi nje ya ofisi ya waziri mkuu wa nchi hiyo baada ya amri mpya ya kuzuia mikusanyiko kuanza kutekelezwa nchini kote.

Muda mfupi tangu kuanza kutekelezwa kwa amri hiyo, polisi wa kutuliza ghasia walisonga mbele na kuwatawanya waandamanaji ambao baadhi walijaribu kuweka vizuizi kwa kutumia chupa na makopo. Hadi alfajiri ya leo polisi walikuwa wakipiga doria katika baadhi ya mitaa ya Bangkok huku wanasheria wa haki za biandamu wakisema viongozi watatu wa maandamano hayo wamekamatwa. Mfululizo wa maandamano ya umma yanayoendelea kwa miezi mitatu sasa, umevutia makumi kwa maelfu ya watu katika mitaa ya mji mkuu Bangkok kushinikiza kujiuzulu kwa Waziri Mkuu Prayuth Chanocha na kuandikwa kwa katiba mpya ya Thailand

Facebook Comments