Mzozo kati ya Armenia na Azerbaijan kushika kasi baada ya kila upande ukiutuhumu mwingine kwa mashambulizi mapya ndani ya jimbo lenye mzozo la Nagorno Karabakh ambalo limeshuhudia mapigano makali kwa muda wa wiki tatu.

Ishara ya kutanuka kwa mzozo huo zimeonekana baada ya jeshi la Azerbaijan kuharibu mfumo wa kufyatua makombora wa Armenia katika mpaka wa nchi hiyo kwa madai kuwa ulilenga kushambulia makaazi ya watu.

Wizara ya ulinzi ya Armenia imesema kutokana na uharibifu uliotokea nchi hiyo inayo haki ya kuilenga miundombuinu ya kivita na wanajeshi wa Azerbaijan.

Wakati hayo yakijiri, Rais Vlamidir Putin wa Urusi alifanya mazunguzmo kwa njia ya simu na mwenzake wa Uturuki Reccep Erdogan na kuhimiza umuhimu wa kuheshimiwa makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyofikiwa Jumapili iliyopita.

Facebook Comments