Watumiaji wa magari, mashine na mitambo inayotumia petroli watalazimika kulipa zaidi kuanzia leo baada ya bei kupanda.


Wakati hali ikiwa hivyo kwa watumiaji wa petroli, wale wa dizeli wana unafuu kutokana na kupungua kwa bei ya nishati hiyo.


Licha ya petroli, taarifa iliyotolewa na kaimu mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura), Godfrey Chibulunje inaeleza kupanda kwa bei ya mafuta ya taa pia.


Kwa mikoa inayotumia Bandari ya Dar es Salaam, bei ya petroli imeongezeka kwa Sh25 na Sh12 kwa lita moja ya mafuta ya taa huku dizeli ikipungua kwa Sh28.07.


Kwa kanda ya Kaskazini ambako mafuta hupitia Bandari ya Tanga, bei ya petroli imeongezeka kwa Sh52 kwa lita moja wakati dizeli ikipungua kwa Sh38 na mafuta ya taa nayo yakipungua kwa Sh7 kwa lita.


Na mikoa ya Kusini inayotumia Bandari ya Mtwara, bei ya petroli imeongezeka kwa Sh10 wakati dizeli ikipungua kwa Sh83.

Facebook Comments