Rais wa Marekani Donald Trump ameendelea kutoa kauli zenye utata kuhusu zoezi zima linaloendelea nchini humo la uhesabuji wa kura katika maeneo mbali mbali ya vituo.

Trump, ameesema kwamba atakwenda kupinga matokeo Mahakamani ili kuzuia zoezi zima linaloendelea la kuhesabu kura.

Trump amenukuliwa akisema,” Tumekwisha shinda uchaguzi huu, lakini kuna hujuma inafanywa dhidi ya Umma wa Marekani”. Kauli hiyo ni mfululizo wa kauli tata ambazo amekua akizitoa mfululizo.

Aidha Trump, ameendelea kuibua mjadala zaidi baada ya kuandika kupitia ukurasa wake wa Twitter kwamba kuna mpango umeandaliwa wa kumuibia kura na wala hataruhusu jambo hilo lifanikiwe.


Matamshi yake yameamsha hisia zaidi nchini humo, huku akiongeza hofu ya kutokea kwa vurugu ikiwa atashindwa katika Uchaguzi huu. Awali alishatangaza kuwa huenda asikubaliane na matokeo ya Uchaguzi ambao anadai kuna njama za kumuibia kura

Twitter imetoa tahadhari kuwa sehemu au chapisho zima la Trump linaweza kuwa la kupotosha kuhusu zoezi la Uchaguzi linaloendelea nchini humo.

Matokeo rasmi yanatarajiwa kutolewa muda wowote kuanzia sasa lakini mchuano bado mkali kati ya Trump na Joe Biden.

Facebook Comments