Dkt. Mwinyi ametoa pongezi hizo leo Novemba 10, Ikulu Jijini Zanzibar wakati alipokutana na uongozi wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), wakiwemo Makamishna wa Tume hiyo wakiongozwa na Mwenyekiti wake Jaji Mstaafu Hamid Mahmoud pamoja na Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Thabit Idarous Faina.

Rais Dkt. Hussein Mwinyi aliueleza amesema ameona haja ya kuwaita viongozi hao baada ya kukamilika kwa mchakato wa uchaguzi kwa azma ya kuwashukuru na kuwapongeza kwa kazi kubwa na nzuri waliyoifanya.

Aidha, Rais Dkt. Hussein amewaahidi viongozi hao kuwa ataendelea kutoa ushirikiano wake kwao na kusisitiza kwamba milango yake iko wazi akimaanisha kwamba yuko tayari kushirikiana nao na kuwasikiliza wakati wowote

Facebook Comments