Vikao vya bunge la 12 vimeanza rasmi jijini Dodoma mapema asubuhi ya leo kwa wabunge wateule kuanza kwa kwa kupiga kura kumchagua Spika wa Bunge hilo ambapo Mh.Job Yustino Ndugai ameshinda kwa kishindo kama ilivyotarajiwa na wengi.

Akisimamia zoezi hilo aliyekua Mwenyekiti wa muda wa kikao hicho alikua ni Mbunge wa Isimani Mh, William Vangimembe Lukuvi ambapo alihakikisha zoezi na Mchakato mzima umeenda salama na Spika kupatikana.

Ndugai amechaguliwa kuwa spika wa Bunge la Tanzania kwa ushindi wa asilimia 99.7. Ndugai aliliongoza bunge hilo akiwa spika kwa kipindi cha miaka mitano, ambapo hii leo akmekitetea kiti chake kwa ajili ya kukitumikia kwa miaka mitano mingine.

Awali Katibu wa Bunge, Stephen Kigaigai alisema kuwa amemuengua Bonaventura Peter Ndekenja wa chama cha NRA aliyemtumia barua pepe akieleza nia yake ya kutaka kuwa Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Zoezi la kuwaapisha baadhi ya wabunge wateule linaendelea bungeni Jijini Dodoma likitarajiwa kuchukua siku kadhaa huku Spika akitahadharisha kwamba Bunge hilo halitakua na Kambi Rasmi ya upinzani kwakua wapinzani wanatakiwa kufikia walau asilimia 12.5 ndipo waweze kuunda kambi hiyo.

Facebook Comments