Rais Mteule wa Marekan i Joe Biden amesema hatua ya Rais Donald Trump kugomea kukubali matokeo ya uchaguzi wa Urais wa wiki iliyopita ni “aibu”.

Lakini kiongozi huyo mteule ambaye amekuwa akiwasiliana na viongozi wa kimataifa – amesisitiza kwamba hakuna kitu kitakachozuia uhamisho wa madaraka.

Huku hayo yakijiri Bw. Trump aliweka ujumbe kwenye mtandao wake wa Twitter akisema atashinda kinyang’anyiro hicho cha uchaguzi ambacho kilibashiriwa na vituo vikuu vya televisheni kwamba atashindwa.

Kama inavyofanyika kila miaka minne, vyombo vya habari vya Marekani hubashiri mshindi.

Mpaka sasa matokeo ya uchaguzi kutoka majimbo ya Marekani hayajaidhinishwa, kura bado zinahesabiwa, lakini matokeo yatatolewa rasmi pindi wajumbe maalum watakapokutana Disemba, 14.

Alipoulizwa na waandishi wa habari siku ya Jumanne kile anachofikiria kuhusu hatua ya Rais Trump kukubali kwamba alishindwa katika uchaguzi alisema.

“Nadhani ni aibu, kusema kweli,” Bw. Biden, mwanachama wa Democratic, alisema mjini Wilmington, Delaware.

“Kile ninachoweza kusema, kwa heshima, Nadhani hatua hiyo haitasaidia kudumisha hadhi ya rais atakapoondoka madarakani.”

“Mwisho wa siku, mbivu na mbichi itajulikana Januari 20,” alisema akiashiria siku ya kuapishwa.

Facebook Comments