Mwenyekiti wa Tume ya taifa ya Uchaguzi Ghana, Jena Mensa, alimetangaza matokeo yauchaguziwa Rais mjini Accra, Ghana.

Rais Nana Akufo Addo, wa Ghana ameshinda uchaguzi mkuu wa nchi hiyo, kwa kupata asilimia 51.6 ya Kura, dhidi mpinzani wake, Rais wa Zamani wa taifa hilo, John Mahama aliyepata asilimia 47.4 ya kura zote.

Hii ni mara ya pili kwa wapinzani hawa wa kisaiasa kukabiliana katika uchaguzi mkuu wa rais.

Rais Nana Akuf- Addo

Rais Akufo Addo ametetea nafasi yake hiyo,dhidi ya mpinzani wake huyo ambaye tangu awali alionyesha wasiwasi wake wa kutumika kwa nguvu ya Jeshi kwenye uchaguzi huo.

Bwana Mahama amelalamikia wizi wa kura.

Awali polisi walisema kulikuwa na kesi 21 wakati wa uchaguzi huo zinazohusiana na ghasia tangu Jumatatu, huku watu watano wakiwa wamefariki.

Rais Akufo Addo amewashukuru raia kwa kumchagua.

Facebook Comments