Muimbaji wa kike wa miondoko ya kufoka(rapper) kutoka nchini Marekani aliyetamba miaka ya 90′ Sandra Pepa, kutoka kundi maarufu la Salt n Pepa, amemshtaki Daktari aliyemfanyia marekebisho ya makalio yake.

Rapper Pepa

Pepa anasema baada ya kupata ajali maumivu yalimuanza na aliamtafuta Dr. David Sayah, ambae alimfanyia marekebisho hayo. Dr.Sayah alimuambia amfanyie upasuaji mwingine tena na kumfanyia upasuaji kwa mara ya tatu ambayo bado ilimfanya makalio yake kuwa magumu hata baada ya kutumia sindano tofauti tofauti alizochomwa na Daktari huyu.

Pepa (54), anasema sasa makalio yake yamepoteza muonekano mzuri na pia akiwa anatumbuiza jukwaani makalio huwa yana muuma kwa hiyo ni lazima ammburuze mahakamani.

Kundi la Salt n’ Pepa

Kundi la Salt n Pepa ni kundi lililovuma sana miaka ya 90′ kwa vibao vya kama Shoop, Let’s talk about sex, Whatta Man, Push it na vingine vingi.

Facebook Comments