Mwanamume mmoja raia wa Kenya ambaye alipata mafunzo ya urubani Ufilipino anatuhumiwa kwa kupanga njama ya kutaka kuteka ndege na kuigongesha kwenye jumba refu la ghorofa katika mji wa Marekani.

Cholo Abdi Abdullah alikamatwa na kushtakiwa baada ya kupatikana na silaha Ufilipino mwisho wa mwaka uliyopita. Waendesha mashtaka hawakutaja ni mji gani alikuwa anadaiwa kupanga kushambulia.

Cholo Abdi Abdullah

Kwa mujibu wa shirika la upelelezi la Marekani FBI, alikuwa akiongozwa na viongozi wa ngazi ya juu katika kundi la kigaidi la al-Shabab lenye makao yake Somalia.

Apingina mashataka yote dhidi yake, ripoti za Shirika la habari la Reuters, zinasema. Advertisement

Wakili wake siku ya Jumatano alikubaliana na jaji kwamba Bw. Abdullah asalie kizuizini akisubiri kusikizwa kwa kesi yake mwezi Januari.

Kwa mujibu wa mashtaka ta FBI ambayo hayakufunguliwa siku Jumatano, Bw. Abdullah, 30, alipelekwa Mrekani baada ya kukamatwa Ufilipino siku ya Jumanne ili afunguliwe mashtaka ya ugaidi, ikiwa ni pamoja na uharamia wa ndege na kula njama za kuwaua raia wa Marekani.

Maafisa wanasema Bw. Abdullah alijiunga na chuo cha urubani nchini Ufilipino mwaka 2016, na kufikia vigezo vyote vinavyohitajika kupata leseni ya urubani “kwa kusudi la kupata mafunzo ya kutekeleza shambulio la mtindo wa 9/11”.

Al-Qaeda-iliongoza shambulio laSeptema 11 mwaka 2001 dhidi ya Marekani- maarufu 9/11 – ambapo ndege ya abiria ilitekwa na kuvurumizwa kwenye majengo mawili kwa wakati mmoja, na kuwaua karibu watu 3,000. Al-Shabab ikishirikiana na al-Qaeda imetekeleza mashambulio kadhaa ya ugaidi Afrika Mashariki.

Wachunguzi wanasema wakati alilopokuwa akipata mafunzo ya urubani, Bw. Abdullah alifanya uchunguzi wa jinsi ya kuvuruga mfumo wa ndege ya kibinafsi, “maelezo kuhusu mijengo mirefu marefu katika miji mikuu ya Marekani,” na jinsio ya kupata visa ya Marekani.

Mpango huo unadaiwa kuwa sehemu ya oparesheni ya al-Shabab “Jerusalem kamwe haitafanywa ya Kiyahudi,” ambayo ilibuniwa kujibu hatua ya utawala wa Trump kuhamisha ubalozi wake nchini Israel katika mji wa Jerusalem.

“Karibi miaka 20 baada ya shambulio la kigaidi la 9/11, kuna wale ambao wamejitolea kufanya vitendo vya kigaidi na ,mashambulio dhidi ya raia wa Marekani ,” alisema Naibu Mkurugenzi wa Msimamizi wa FBI William F Sweeney Jr.

“[Bw.] Abdullah, alidaiwa kuwa mmoja wao. Alipata leseni ya urubani ughaibuni, kujifunza namna ya kuteka ndege kwa lengo la -kudhuru watu ndani ya mipaka yetu.”

Wachunguzi pia wanasema Bw. Abdullaha alipikuwa anaongozwa na maafisa wa ngazi ya juu wa al-Shabab ambao walipanga mashambulio ya mwaka 2019 dhidi ya hoteli ya kifahari katika mji mkuu wa Nairobi nchini Kenya.

Facebook Comments