Spika wa bunge la uwakilishi nchini Marekani Nancy Pelosi, ametoa rasmi na kuwapatia wabunge mpango wa jinsi ya kumuondoa rais Donald Trump kutoka ofisini kabla ya kuanza kwa mchakato wa kumshtaki.

Bunge la uwakilishi litapiga kura kuhusu maamuzi yanayomtaka makamu wa rais Mike Pence kuondoa mamlaka ya urais ya bwana Trump.

Iwapo hatua hiyo itafeli , Democrats watawasilisha mashtaka ya uasi dhidi ya rais Trump kuhusu jukumu lake la uvamizi wa jumba la Capitol Hill.

Kura ya kwanza huenda ikapigwa siku ya Jumatatu.

Siku ya Jumapili , bi Pelosi aliwaandikia wabunge akielezea mpango wa maamuzi ya kumtaka makamu wa rais Mike Pence kutumia kifungu cha sheria cha 25 kitakachomuwezesha kuwa rais wa muda uliosalia.

Hatua hiyo itamruhusu Pence kuwa kaimu rais na kumuondoa Trump katika Ikulu ya Whitehouse.

Nancy Pelosi

Kiranja wa bunge James Clyburn aliambia CNN kwamba hatua zitachukuliwa wiki hii.

Lakini chama hicho huenda kisitumie kifungu chochote cha sheria katika bunge la seneti ili kumfungulia mashtaka hayo hadi rais mteule Joe Biden atakapohudumu siku zake 100 za kwanza afisini.

Hatua hiyo itamruhusu bwana Biden kuthibitisha baraza lake jipya la mawaziri na kuanzisha sera muhimu ikiwemo kukabiliana na virusi vya corona kitu ambacho kitalazimika kusubiri iwapo bunge la seneti litakuwa limepokea vifungu hivyo vya kumshtaki rais Donald Trump.

Donal Trump

Bwana Trump ameshutumiwa na wanachama wa Democrats na idadi ndogo ya wanachama wa Republican kwa kuchochea ghasia za Jumatano iliopita ambapo takriban watu watano walifariki.

Lakini hakuna hata mwanachama mmoja wa Republican amesema kwamba atapiga kura ya imani dhidi yake kwa makosa hayo katika seneti.

Seneta wa pili wa chama cha Republican Pat Toomey alimtaka rais Trump kujiuzulu siku ya Jumapili.

”Nadhani njia bora kwa taifa letu …ni kwa rais kujiuzulu na kuondoka haraka iwezekanavyo”, alisema Seneta Toomey akizungumza na chombo cha habari cha NBC.

Lisa Murkowski, kutoka jimbo la Alaska, alikuwa seneta wa kwanza wa Republican kumwambia rais kuondoka mmamlakani .

Wakati huohuo aliyekuwa seneta wa California Arnold Schwarzenegger alimtaja rais Trump kuwa rais mbaya zaidi katika video moja ya mtandaoni.

Ikulu ya Whitehouse imepuuzilia mbali kura hiyo ya maoni kama inayochochowa kisiasa hatua ambayo huenda ikazidisha mgawanyiko unaoshuhudiwa nchini humo.

Iwapo mpango huo utaendelea , bwana Trump huenda akawa rais wa kwanza katika historia ya Marekani kushtakiwa na bunge mara mbili.

Facebook Comments