Iran imeilaumu Marekani kwa kuingilia masuala ya ndani ya Cuba baada ya kisiwa hicho chenye utawala wa kikomunisti kukumbwa na maandamano makubwa.

Kisiwa hicho cha Cuba kimewekewa vikwazo na Marekani kwa miongo kadhaa sasa. Katika taarifa iliyotolewa na msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Iran, Saeed Khatibzadeh, amesema Marekani kwa sasa inawaunga mkono waandamanaji wa Cuba wakati ambapo inahusika na matatizo mengi wanayoyapitia raia wa Cuba.

Iran yenyewe imewekewa vikwazo na Marekani. Maandamano nchini Cuba yalianza ghafla siku ya Jumapili katika miji kadhaa huku Cuba ikiwa inapitia mgogoro mkubwa kabisa wa kiuchumi katika kipindi cha miaka 30 huku nchi hiyo ikikumbwa na upungufu mkubwa wa umeme, chakula na madawa.

Facebook Comments