Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Injinia Hersi Said ametuma ujumbe mrefu wa kumuaga kiungo wao mshambuliaji Haruna Niyonzima ambaye anaondoka klabuni hapo baada ya kumalizika kwa msimu huu wa 2020/21, lakini ametupa jiwe gizani.

Injinia ametaja kuwa Yanga haina kawaida ya kuwashutumu wachezaji wake kuwa wana matatizo ya akili.

Licha ya kutotaja jina lakini ikumbukwe ni hivi karibuni Klabu ya Simba kupitia Kamati ya Nidhamu ilimuweka pembeni kwa muda kiungo Jonas Mkude na kutakiwa kwenda hospitali kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya kabla ya kutoa hukumu ya masuala yake ya kinidhamu yaliyokuwa yakimkabili.

TAMKO KAMILI YA INJINIA ALILOTOA KUPITIA UKURASA WAKE WA INSTAGRAMA HILI HAPA CHINI…

Farewell, from fare wel!, an imperative expression, possibly further derived from Old English *far wel!, equivalent to fare (“to fare, travel, journey”) +‎ well. Compare Scots farewele, fairweill (“farewell”), kwa ufupi, waarabu wanasema توديع – فراق

Heshima ya kuitumikia klabu kubwa yenye kujali watumishi wake ni kuagana kwa wema mnapofikia muafaka wa musqbal wao kwa pamoja.

Tumekuwa na kipindi kizuri kwa pamoja katika mahusiano ya kimkataba yaliyoleta faida kwa pande zote mbili.

Ustadi wako uwanjani ulikufanya uimbwe na kila mpenda soka safi na hata kunasibishwa na Cesc FABRIGAS, mmoja kati ya viungo bora kupata kutokea katika karne hii.

Ubora wa kuwa kiongozi ndani na nje ya uwanja umekufanya uvae USINGA na kupewa jukumu la kuongoza jahazi la WANANCHI katika mafanikio.

Nakumbuka ilikuwa 19th DECEMBER 2019 tulipokutana MARRIOTT HOTEL – KIGALI na kukubaliana urudi JANGWANI kuleta burudani kwa wananchi, hukusita na ukamwaga wino katika karatasi za KIJANI na NJANO!

Malengo yalikuwa mawili, kuleta kiwango uwanjani na muongozo kwa wenzako nje ya uwanja.

Ama hakika ulikuwa HARUNA MPYA wa kuitwa “the problem solver” na sio “the problem maker”

@niyonzimaharuna I am 100% sure u have few more years to play before you hang up ur boots!

Nenda kacheze na umalizie ufundi wako uliojaaliwa na mola mwenyezi.

Mwisho na sio kwa umuhimu, WANANCHI tukimalizana na wachezaji wetu huwa hatuwapi kashfa za kuwa WANAKICHAA na kuwapeleka MIREMBE, tunawaaga kwa HESHIMA!

THANK 8 YOU @niyonzimaharuna

Facebook Comments