Winga na mshambuliaji Mtanzania Simon Msuva @smsuva27 amefanikiwa kubeba ubingwa wa Ligi Kuu ya Morocco akiwa na kikosi cha Wydad Casablanca.

Timu hiyo imebeba taji la Morocco 2020/21 baada ya kuifunga MCO Oudja mabao 2-0.

Wydad wamebeba taji hilo wakiwa na michezo mitatu mkononi, wamefikisha pointi 63 katika mechi 27.

Facebook Comments