Kampuni ya Google na Facebook yamewataka wafanyakazi wake kuchanjwa kabla ya kurejea ofisini, taarifa hiyo inakuja baada ya kupita miezi 16 ya wafanyakazi kuendesha shughuli zao wakiwa nyumbani kutokana na mlipuko wa Ugonjwa wa COVID-19.

C.E.O wa Google, Sundar Pichai ametoa taarifa hiyo kwenye e-mail iliyotumwa kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo, ambayo inaeleza juu ya umuhimu wa kupata chanjo ili kujikinga na kuikinga jamii nzima kutokana mlipuko wa wimbi la tatu la COVID-19.

Wakati Makamu wa Rais wa Facebook, Lori Goler amewataka wafanyakazi kwa yeyote anayetaka kuingia ofisini lazima awe amepata chanjo ya COVID-19.

Hii inafanya makampuni haya kuwa ya kwanza kuja na uamuzi huo wakati makampuni mengine yakiwaza jinsi ya kurudisha wafanyakazi ofisini wakati ambapo kirusi delta COVID-19 kikiendelea kuwa tishio duniani kote.

Na Noel Martnes Moddy @scopeboiii

Facebook Comments