Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako yuko nchini Uingereza kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Washirika Wafadhili wa Elimu Duniani, Global Partnership In Education GPE.

Akiwa nchini humo Julai 28, 2021 amekutana na kufanya mazungumzo na majadiliano na viongozi mbalimbali kuhusu masuala ya mabadiliko ya tabia nchi na Athari zake katika utoaji elimu, ushiriki wa vijana katika kupambana na mabadiliko ya nchi na utekekezaji wa mradi wa shule bora ambao utajenga shule za bweni 13 za wasichana nchini.

Viongozi aliokutana nao ni pamoja na Waziri wa Elimu wa Uingereza, Gavin Williamson, Lord Ahmad Waziri anaeshughulikia masuala ya Asia Kusini katika Ofisi ya Jumuiya na Madola na Ushirikiano wa Kimataifa pamoja na Mhe Duddridge Waziri anaeshughulikia Masuala ya Afrika katika Ofisi ya Jumuiya ya Madola.

@ikulu_mawasiliano @gersonmsigwa @habarileotsn @uhurudigital_tz @msemajimkuuwaserikali @maelezonews @prof_joyce_ndalichako @akwilapo@ikuluzanzibar@gpforeducation @dfid_uk @johnharamba

TimesFMDigital #TimesFmNiBaraka #HujasikiaBado #MgusoWaJamii

Facebook Comments