Mtoto aliyezaliwa akiwa na uzito ambao ni sawa uzito wa tufaha (apple) ameruhusiwa kutoka Hospitali ya Singapore baada ya matibabu na uangalizi maalumu wa madaktari kwa muda wa mwezi 13.

Mtoto huyo alizaliwa akiwa mchanga zaidi akiwa na gramu 212 tu wakati wa kuzaliwa, sasa ana uzito wa 6.3Kg na ameruhusiwa kutoka hospitali.

Ingawa mtoto huyo (Yu Xuan) bado ana ugonjwa wa mapafu, atahitaji msaada kwa kupumua wakati akiwa nyumbani, lakini madaktari wamesema atapata nafuu na kuwa sawa.

#TimesFMDigital#TimesFmNiBaraka#HujasikiaBado#mgusowajamii📻🎧🎤🔥🔥🔥

Facebook Comments