Kikosi cha Simba kimeingia kabini kwa ajili ya kuanza maandalizi ya kuelekea kwenye msimu ujao wa 2021/22, ambapo kuna uwezekano wa kambi yao kuiweka nchini Morocco.

Kiungo Jonas Mkude na winga Perfect Chikwende ni baadhi ya wachezaji ambao wameshawasili kambini, wawili hao walikosa mechi nyingi kuelekea mwishoni mwa msimu uliopita kutokana na sababu tofauti.

Mkude alikosa mechi nyingi kutokana na matatizo ya kinidhamu wakati Chikwende alikosa nafasi katika kikosi cha kwanza kutokana na ushindani mkali.

#TimesFMDigital#TimesFmNiBaraka#HujasikiaBado#mgusowajamii📻🎧🎤🔥🔥🔥

Facebook Comments