Mara baada ya kushuhudia kutoka kwa albamu ya Kanye West “DONDA” jumapili ya wiki iliyopita, huenda tukashuhudia albamu nyingine kutoka mwishoni mwa wiki hii, kutoka kwa mkali wa muziki wa rap Drizzy Drake.

Albamu hiyo imepewa jina la “CERTIFIED LOVER BOY” na inatarajiwa kuachiwa Ijumaa ya Septemba 03, 2021.

Kupitia Insta story ya Champagne Papi alichapisha andiko lifuatalo kutoka kwenye bango la matangazo “Billboard” lililobeba miongoni mwa maudhui kutoka kwenye albamu hiyo.

“Ilipaswa kusema unanipenda leo, kwa sababu kesho ni siku mpya” ujumbe uliendelea kwa kusema “Sijihisi kukosa, Acha upekee uhisi kukukosa” @ChampagnePapi ✍️

Unadhani albamu ya DRAKE “Certified Lover Boy” itaweza kuzivunja rekodi za albamu ya KANYE WEST “DONDA”?

#TimesFMDigital#TimesFmNiBaraka#HujasikiaBado#MgusoWaJamii

Facebook Comments