Kufuatia sakata la Mbunge wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima na Bunge, Spika wa Bunge, Job Ndugai ametoa kauli hii:

“Kuhusu Gwajima sisi hapa hatujamshitaki kama askofu, tumemshtaki kama Mbunge Gwajima, habari za uaskofu wake ni hukohuko, unaweza ukawa askofu halafu kama wenzako hawaelewi dini siyo hivyo hayo ni macho ya makengeza watu ni waumini sana.

“Mimi ni Mzee wa Kanisa la Anglikana wa miaka mingi, ni nafasi ya Mshauri wa Askofu, nimeshakwenda Nigeria kwa TB Joshua, nimeenda Makao Makuu ya Kanisa langu, Uyahudi nimekwenda mara nne, nimeenda kwenye Kijiji cha Yesu, Galilaya yote ile nilitembea naijua.

“Nimefika Nazareth, mara ya mwisho nimeenda na Mwalimu Mwakasege, tunatamba sisi? Sasa ukiwa askofu utudanganye sisi? Dini tunaijua, mnavyokwenda siyo kutumia platform ya dini kila Jumapili kuhamasisha

“Mtusikilize, mtasikia mabomu kesho, Waziri wa Mambo ya Ndani uko hapa, Serikali mko hapa hii haiwezi kwenda hivi.”

#TimesFMDigital #TimesFmNiBaraka #HujasikiaBado #MgusoWaJamii

Facebook Comments