Baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge, Emmanuel Mwakasaka kutoa ripoti ya kamati hiyo kuhusu hatia walizokutwa nazo wabunge Josephat Gwajima na Jerry Silaa, hatimaye Spika Job Ndugai ametoa tamko.

Kwanza amemtoa bungeni Mbunge wa Ukonga, Jerry Silaa na kuhusu Gwajima alikuwa na haya ya kusema:

“Gwajima hayupo, Silaa yupo sasa naomba Silaa utoke nje tutaonana January,2022 na Sajenti naomba mtoke naye nje ya viunga vya Bunge.

“Katika kipindi hiki ambacho wamesimamishwa hawataruhusiwa kukanyaga maeneo ya Bunge isipokuwa kwa ridhaa ya Spika na watapata nusu ya mshahara na nusu ya mambo mengine ambayo watastahili kuyapata hivyo ndivyo kanuni zinavyosema.”

#TimesFMDigital #TimesFmNiBaraka #HujasikiaBado #MgusoWaJamii

Facebook Comments