Search in the website:

Author: guest01 / Page 2

HAKUNA KUINGIA GOOGLE, FACEBOOK BILA CHANJO YA CORONA

Written by on 29 July 2021

Kampuni ya Google na Facebook yamewataka wafanyakazi wake kuchanjwa kabla ya kurejea ofisini, taarifa hiyo inakuja baada ya kupita miezi 16 ya wafanyakazi kuendesha shughuli zao wakiwa nyumbani kutokana na mlipuko wa Ugonjwa wa COVID-19. C.E.O wa Google, Sundar Pichai ametoa taarifa hiyo kwenye e-mail iliyotumwa kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo, ambayo inaeleza juu ya […]

Read More

MABADILIKO YA TABIA NCHI YAMPELEKA NDALICHAKO UINGEREZA

Written by on 29 July 2021

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako yuko nchini Uingereza kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Washirika Wafadhili wa Elimu Duniani, Global Partnership In Education GPE. Akiwa nchini humo Julai 28, 2021 amekutana na kufanya mazungumzo na majadiliano na viongozi mbalimbali kuhusu masuala ya mabadiliko ya tabia nchi na Athari zake katika utoaji elimu, ushiriki […]

Read More

MIKOA 10 KIPAUMBELE CHANJO CORONA

Written by on 26 July 2021

Serikali imepokea msaada wa chanjo ya Corona kutoka Marekani na kueleza kuwa baada ya kujiridhisha kuwa ni salama utolewaji wake utafanyika nchi nzima lakini kwa kuanza na mikoa 10 ya kipaumbele. Mikoa hiyo ya kipaumbele ni Dar es Salaam, Mwanza, Kilimanjaro, Mbeya, Arusha, Kigoma, Singida, Dodoma, Iringa na Mtwara. Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, […]

Read More

WYDAD YA MSUVA YABEBA UBINGWA WA MOROCCO

Written by on 15 July 2021

Winga na mshambuliaji Mtanzania Simon Msuva @smsuva27 amefanikiwa kubeba ubingwa wa Ligi Kuu ya Morocco akiwa na kikosi cha Wydad Casablanca. Timu hiyo imebeba taji la Morocco 2020/21 baada ya kuifunga MCO Oudja mabao 2-0. Wydad wamebeba taji hilo wakiwa na michezo mitatu mkononi, wamefikisha pointi 63 katika mechi 27.

Read More

RWANDA YAIWEKA KIGALI LOCKDOWN KWA SIKU 10

Written by on 15 July 2021

Serikali ya Rwanda imetangaza ‘lockdown’ ya siku 10 katika Jiji la Kigali na wilaya nane baada ya kuongezeka visa na vifo vya raia vilivyotokana na maambukizi ya Virusi vya Corona. Raia nchini humo wametakiwa kukaa ndani kuanzia Jumamosi Julai 17 hadi Julai 26, 2021 ili kuzuia kuenea kwa maambukizi ya ugonjwa huo. Katika masharti hayo […]

Read More

HII NDIYO TOFAUTI YA NIYONZIMA Vs OKWI

Written by on 15 July 2021

Haruna Niyonzima anatarajiwa kuondoka Yanga hivi karibuni, klabu hiyo ya Jangwani imeamua kumpa heshima kubwa ya kumuaga, hakika alistahili. Naamini licha ya kucheza Simba lakini bado ukiuliza shabiki yeyote wa soka kuwa Niyonzima ni shujaa wa wapi, atakwambia ni wa Yanga, ndiyo ni hivyo kwa kuwa muda mrefu aliodumu klabuni hapo ulimtengenezea ‘chemistry’ kati yake […]

Read More

INJINIA: YANGA HATUWAPI WACHEZAJI WETU KASHFA YA UKICHAA

Written by on 15 July 2021

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Injinia Hersi Said ametuma ujumbe mrefu wa kumuaga kiungo wao mshambuliaji Haruna Niyonzima ambaye anaondoka klabuni hapo baada ya kumalizika kwa msimu huu wa 2020/21, lakini ametupa jiwe gizani. Injinia ametaja kuwa Yanga haina kawaida ya kuwashutumu wachezaji wake kuwa wana matatizo ya akili. Licha ya kutotaja jina lakini ikumbukwe ni […]

Read More

IRAN YAITUHUMU MAREKANI KUINGILIA MASUALA YA CUBA

Written by on 14 July 2021

Iran imeilaumu Marekani kwa kuingilia masuala ya ndani ya Cuba baada ya kisiwa hicho chenye utawala wa kikomunisti kukumbwa na maandamano makubwa. Kisiwa hicho cha Cuba kimewekewa vikwazo na Marekani kwa miongo kadhaa sasa. Katika taarifa iliyotolewa na msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Iran, Saeed Khatibzadeh, amesema Marekani kwa sasa inawaunga mkono […]

Read More

Load more