the QUARTZ Blog

Nahreel & Aika wamchukua director wa Uganda,Lukyamuzi Bashir kufanya video mpya 'We Do Work'

posted 1 year ago by admin

Wanamuziki wa kundi la Navy Kenzo (Nahreel & Aika) ambao wanazidi kupasua anga Afrika Mashariki,wameamua kumchukua muongozaji wa video raia wa Uganda 'Lukyamuzi Bashir' kufanya video yao mpya 'We Do Work'

Lukyamuzi Bashir ni muongozaji ambaye ameshawahi kufanya vizuri kwenye video mbalimbali nchini Uganda ikiwemo ya Jose Chamilione 'Valu Valu'

Nahreel akiongea na 100.5 anasema walipata nafasi ya kufanya kazi na muongozaji huyo baada ya kumaliza ziara yao nchini Uganda.

'Sisi tulikutana na Lukyamuzi Bashir kipindi tulipokuwa kiziara nchini Uganda ndipo tukaamua kufanya naye kazi kwani lengo letu tubadilishe utofauti wa kazi zetu na kuzidi kupendwa na mashabiki,tumefanya naye video ya wimbo mpya 'We Do Work' ambao tunatarajia kutambuliza rasmi Sept 28 katika vituo mbalimbali'alisema Nahreel

Kwa hiyo kama wewe ni shabiki wa kundi la Navy Kenzo basi kaa tayari kwa ujio wa video ya wimbo wao mpya 'We Do Work'

comments powered by Disqus