Search in the website:

Uncategorized

Rapa Pepa amshtaki Daktari kwa kumharibu makalio

Written by on 14 December 2020

Muimbaji wa kike wa miondoko ya kufoka(rapper) kutoka nchini Marekani aliyetamba miaka ya 90′ Sandra Pepa, kutoka kundi maarufu la Salt n Pepa, amemshtaki Daktari aliyemfanyia marekebisho ya makalio yake. Pepa anasema baada ya kupata ajali maumivu yalimuanza na aliamtafuta Dr. David Sayah, ambae alimfanyia marekebisho hayo. Dr.Sayah alimuambia amfanyie upasuaji mwingine tena na kumfanyia […]

Read More

MICHEZO: SENZO MBATHA ASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI NCHINI, KISA?

Written by on 11 November 2020

Senzo Mbatha anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwenye kituo cha Polisi Oysterbay. Inaelezwa sababu ya Senzo kushikiliwa na jeshi la polisi ni kuhusiana na tuhuma za mawasiliano yake na Hashim Mbaga yanayodhaniwa yalilenga kuihujumu Simba (kupanga matokeo) kwenye michezo kadhaa. Hivi karibuni Hashim Mbaga (aliyekuwa Mkurugenzi wa Wanachama na Mashabiki-Simba) alikamatwa na Jeshi la Polisi […]

Read More

SERIKALI: HATUJAPATA TAARIFA YA UN KUHUSU KUUAWA NA KUKAMATWA KWA WAPINZANI

Written by on 11 November 2020

Katibu Mkuu wa Wizara ya Sheria na Katiba, Prof. Sifuni Mchome amesema Serikali haijapokea taarifa ya Umoja wa Mataifa (UN) akiongeza kuwa, watu hao wamekamatwa kisheria. Kupitia tovuti yao, Kamishna wa Shirika la┬áHaki Za Binadam┬ála UN, Michelle Bachelet, alitoa taarifa iliyodai Wapinzani na wafuasi wao 150 wamekamatwa tangu Oktoba 27. Prof. Mchome amesisitiza Serikali haina […]

Read More

LISSU ATIMKIA UBELGIJI

Written by on 11 November 2020

Kiongozi wa upinzani na ambaye alikuwa mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Chadema katika uchaguzi wa Oktoba 28 Tundu Lissu ameondoka nchini Tanzania Jumanne (Jana) kuelekea nchini Ubelgiji. Lissu ambaye alikuwa katika hifadhi ya ubalozi wa Ujerumani nchini Tanzania kwa karibu wiki nzima alianzia safari yake kutokea makazi ya ubalozi kuelekea uwanja wa […]

Read More

BIDEN: “TRUMP ANATIA AIBU”

Written by on 11 November 2020

Rais Mteule wa Marekan i Joe Biden amesema hatua ya Rais Donald Trump kugomea kukubali matokeo ya uchaguzi wa Urais wa wiki iliyopita ni “aibu”. Lakini kiongozi huyo mteule ambaye amekuwa akiwasiliana na viongozi wa kimataifa – amesisitiza kwamba hakuna kitu kitakachozuia uhamisho wa madaraka. Huku hayo yakijiri Bw. Trump aliweka ujumbe kwenye mtandao wake […]

Read More

ETHIOPIA: MAPIGANO YAZIDI KUSHIKA KASI, WANANCHI WATAFUTA HIFADHI SUDAN

Written by on 11 November 2020

Mapigano makali yanaendelea Tigray, Ethiopia, wakimbizi wakikimbilia Sudan huku Umoja wa Afrika ukiendelea kutoa wito wa kusitishwa mapigano hayo. Jeshi la Ethiopia linaendelea kushambulia makundi ya wapiganaji katika eneo hilo, baada ya viongozi wa Tigray kukaidi mamlaka ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed. Karibu watu 2,500 wamekimbilia Sudan kutoka Ethiopia kufuatia mapigano hayo katika eneo la […]

Read More

RAIS WA ZANZIBAR DKT.HUSSEIN ALLY MWINYI AMETOA SHUKRANI NA PONGEZI KWA TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR, ZEC

Written by on 10 November 2020

Dkt. Mwinyi ametoa pongezi hizo leo Novemba 10, Ikulu Jijini Zanzibar wakati alipokutana na uongozi wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), wakiwemo Makamishna wa Tume hiyo wakiongozwa na Mwenyekiti wake Jaji Mstaafu Hamid Mahmoud pamoja na Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Thabit Idarous Faina. Rais Dkt. Hussein Mwinyi aliueleza amesema ameona haja ya kuwaita […]

Read More

VIKAO VYA BUNGE LA 12 VYAANZA KWA WABUNGE WATEULE KULA KIAPO.

Written by on 10 November 2020

Vikao vya bunge la 12 vimeanza rasmi jijini Dodoma mapema asubuhi ya leo kwa wabunge wateule kuanza kwa kwa kupiga kura kumchagua Spika wa Bunge hilo ambapo Mh.Job Yustino Ndugai ameshinda kwa kishindo kama ilivyotarajiwa na wengi. Akisimamia zoezi hilo aliyekua Mwenyekiti wa muda wa kikao hicho alikua ni Mbunge wa Isimani Mh, William Vangimembe […]

Read More

TRUMP AMTIMUA WAZIRI WA ULINZI

Written by on 10 November 2020

Rais Donald Trump amemfuta kazi Waziri wa Ulinzi Mark Esper, na kutangaza kwenye mtandao wa Twitter kwamba afisa huyo wa ngazi ya juu wa Marekani “amefutwa”. Christopher Miller, mkuu wa sasa wa Kituo Cha Kukabiliana na ugaidi amechukua nafasi hiyo mara moja. Hii ni baada ya wawili hao kutofautiana hadharani katika wiki za hivi karibuni. […]

Read More