Search in the website:

Mguso Wa Jamii

Blog with Sidebar / Page 3

BEI YA PETROLI YAPANDA KUANZIA LEO

Written by on 4 November 2020

Watumiaji wa magari, mashine na mitambo inayotumia petroli watalazimika kulipa zaidi kuanzia leo baada ya bei kupanda. Wakati hali ikiwa hivyo kwa watumiaji wa petroli, wale wa dizeli wana unafuu kutokana na kupungua kwa bei ya nishati hiyo. Licha ya petroli, taarifa iliyotolewa na kaimu mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji […]

Read More

TRUMP AJITANGAZA MSHINDI HUKU AKISEMA ATAKWENDA MAHAKAMANI

Written by on 4 November 2020

Rais wa Marekani Donald Trump ameendelea kutoa kauli zenye utata kuhusu zoezi zima linaloendelea nchini humo la uhesabuji wa kura katika maeneo mbali mbali ya vituo. Trump, ameesema kwamba atakwenda kupinga matokeo Mahakamani ili kuzuia zoezi zima linaloendelea la kuhesabu kura. Trump amenukuliwa akisema,” Tumekwisha shinda uchaguzi huu, lakini kuna hujuma inafanywa dhidi ya Umma […]

Read More

VUTA NIKUVUTE UCHAGUZI MKUU MAREKANI

Written by on 4 November 2020

Rais Donald Trump na mpinzani wake Joe Biden wanachuana vikali katika uchaguzi wa Rais uliofanyika jana nchini Marekani katika wakati vituo vya kupigia kura vikiendelea kufungwa na matokeo ya kwanza yakiendelea kutolewa. Vyombo vya habari vimeripoti kuwa Trump amepata ushindi kwenye majimbo ya Alabama, Arkansas, Indiana, Kentucky, Mississippi, Oklahoma, Tennessee na West Virginia, ambayo yote […]

Read More

KOCHA WA WALES RYAN GIGGS AKAMATWA NA POLISI

Written by on 3 November 2020

Ryan Giggs ambae ndio kocha mkuu wa kikosi cha Wales na mchezaji wa zamani wa Manchester United ,amekamatwa na Polisi kwa kosa la kumpiga na kumtukana mpenzi wake Kate Greville, siku ya jumapili. Tukio hilo lilitokea Jumapili majira ya saa kumi alasiri huko nyumbani kwa Giggs Worsley, Ireland. Kufuatia mashtaka hayo usiku wa jana Wakala […]

Read More

UPINZANI WASHINDA URAIS SEYCHELLES

Written by on 26 October 2020

Kiongozi wa Upinzani katika taifa dogo la visiwa vya Shelisheli Wavel Ramkalawan ameshinda uchaguzi wa Rais baada ya tume ya uchaguzi kutangaza matokeo rasmi jana Jumapili. Mwanasiasa huyo mwenye umri wa maiak 59 ambaye pia ni kasisi wa kanisa la Anglikana amepata asilimia 54.9 ya kura na kufanikiwa kumwaondoa madarakani Rais wa sasa Danny Faure. […]

Read More

AFGHANISTAN YASEMA IMEMUUA KIONGOZI MWANDAMIZI WA AL QAEDA

Written by on 26 October 2020

Afghanistan imedai kwamba imemuua kiongozi muhimu wa kundi la al-Qaeda aliye kwenye orodha ya watu wanaotafutwa zaidi na shirika la ujasusi la Marekani FBI. Inatajwa kuwa Husam Abd al-Rauf aliuliwa wakati wa operesheni iliyofanywa na vikosi vya Afghanistan mashariki mwa nchi hiyo, hali inayoashiria uwepo wa wanamgambo hao nchini humo katika wakati wanajeshi wa Marekani […]

Read More

Load more