Search in the website:

Mguso Wa Jamii

Blog with Sidebar / Page 5

VURUGU NIGERIA: RAIS BUHARI ATAKA UTULIVU

Written by on 22 October 2020

Rais Muhammadou Buhari wa Nigeria ametoa wito wa kuwepo utulivu baada ya wanajeshi kuwafyatulia risasi waandamanaji katika mji mkuu wa kibiashara wa Lagos Jumanne usiku. Wito wa Rais umetolewa muda mfupi tu baada ya Gavana wa Jimbo la Lagos kukanusha kuuawa kwa waandamanaji waliokuwa wanakaidi amri ya kutotoka nje, lakini akikiri kwamba karibu waandamanaji 30 […]

Read More

BUYOYA APUUZIA HUKUMU YAKE YA KIFUNGO CHA MAISHA GEREZANI

Written by on 22 October 2020

Rais wa zamani wa Burundi, Pierre Buyoya amesema kuwa amekataa hukumu ya kifungo cha maisha jela aliyopewa bila kuwa mahakamani wiki hii kuhusiana na mauaji ya mwaka wa 1993 ya mtangulizi wake. Buyoya ameipuuzilia mbali kesi hiyo akisema ilichochewa kisiasa. Alihukumiwa Jumatatu na mahakama moja nchini Burundi kwa “shambulizi dhidi ya kiongozi wa taifa” kuhusu […]

Read More

IGP: MAGAIDI ZAIDI YA 300 WALIVAMIA MTWARA

Written by on 22 October 2020

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania IGP Simon Sirro amesema magaidi zaidi ya 300 kutoka Msumbiji walivamia Kijiji cha Kitaya Mkoani Mtwara na kufanya uhalifu ikiwemo mauaji. Vyombo vya habari vy ndani ya Tanzania ikiwemo Jamii Forums na Mwanahalisi Digital vinaripoti kuwa IGP Sirro ameeleza kuwa wahalifu hao waliowajeruhi vijana watano kwa baadhi yao […]

Read More

JE, WAJUA KUWA WAPIGA KURA WANA HAKI YA KUOMBA KARATASI NYINGINE YA KUPIGIA KURA ENDAPO ITATOKEA AMEKOSEA KWA BAHATI MBAYA?

Written by on 22 October 2020

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetoa ufafanuzi wa utaratibu wa upigaji kura katika uchaguzi mkuu na kusema mpiga kura aliyeharibu kwa bahati mbaya karatasi ya kupigia kura akiwa kwenye kituturi kwenye kituo cha kupigia kura, anaweza kuirudisha karatasi hiyo kwa msimamizi wa kituo na kuomba apewe nyingine ili apige kura yake vizuri. Hayo yalisemwa […]

Read More

WAZIRI WA AFYA WA UJERUMANI AKUTWA NA CORONA

Written by on 22 October 2020

Waziri wa Afya wa Ujerumani, Jens Spahn amethibitishwa kukutwa na Virusi vya Corona na tayari ameshajitenga huku watu aliokutana nao wakijulishwa kuhusu hali yake. Spahn ni mmoja kati ya wanasiasa wakubwa wa Ujerumani kukutwa na Virusi hivyo. Uwiano wa maambukizi ya COVID19 umefikia watu 50 kati ya 100,000. Ujerumani imerekodi visa 11,287 ndani ya saa 24 zilizopita na kufanya jumla […]

Read More

Load more