Search in the website:

Mguso Wa Jamii

Blog with Sidebar / Page 6

ISRAEL, EMARATI ZAKUBALIANA

Written by on 21 October 2020

Israel na Umoja wa Falme za Kiarabu, UAE, zimekubaliana juu ya utaratibu wa kusafiri baina yao bila kuhitaji viza, Mkataba wa kwanza kati ya Israel na taifa la Kiarabu, ulisainiwa wakati ujumbe wa kwanza rasmi wa maafisa wa UAE, Emarati, ukiwasili mjini Tel Aviv. Ziara ya ujumbe huo, iliyosifiwa kama siku nzuri ya amani na […]

Read More

TANZANIA YAKOPA ZAIDI YA BIL.100 KUPAMBANA NA CORONA

Written by on 21 October 2020

Benki ya maendeleo ya Afrika imepitisha mkopo wa dola za kimarekani milioni 50.7 sawa na zaidi ya bilioni 117 za kitanzania kugharamia mapambano dhidi ya Covid. Serikali inayoongozwa na Rais John Magufuli inapanga kujenga uthabiti wa kiuchumi na kupunguza athari za kiuchumi, kijamii na kiafya zinazotokana na Covid hasa biashara, kaya zilizo katika hali hatarishi […]

Read More

RAIS WA ZAMANI WA BURUNDI AHUKUMIWA

Written by on 21 October 2020

Mahakama ya juu nchini Burundi imemhukumu kifungo cha maisha aliyekuwa Rais wa taifa hilo Pierre Buyoya kwa madai ya kuhusika na mauaji ya mrithi wake Melchior Ndadaye. Buyoya  ambaye ana umri wa miaka sabini, kwa sasa ni mjumbe wa muungano wa Afrika katika eneo la Sahel. Hajawahi hudhuria vikao vya kesi hiyo ambayo mwaka uliopita aliitaja […]

Read More

VURUGU NA MAANDAMANO NIGERIA, WAWILI WAJERUHIWA

Written by on 21 October 2020

Watu wawili wamejeruhiwa hapo jana mjini Lagos, Nigeria, baada ya wanajeshi kuwafyatulia risasi za moto waandamanaji wanaopinga ukatili wa polisi, kulingana na mashuhuda. Taarifa hizo ni kulingana na mashuhuda wanne waliozungumza na shirika la habari la Reuters. Hata hivyo Jeshi la Nigeria limedai kuwa wanajeshi wake hawakuweko katika eneo hilo la maandamano siku ya Jumanne. […]

Read More

ACT WAZALENDO YAMKANA MEMBE

Written by on 20 October 2020

Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Maalim Seiff Shariff Hamad ameeleza kusikitishwa kwake na kauliĀ  aliyozungumza mgombea Urais wa Chama hicho Bernard Membe akisema kwamba wakati wanampokea walisha mueleza juu ya mashirikiano yao na vyama makini vya siasa ukiacha CCM. Maalim ameeleza kwamba ni afadhali ya Hashim Rungwe mgombea urais wa chama cha ukombozi wa […]

Read More

POLISI NCHINI UFARANSA YAFANYA MSAKO WA MAKUNDI YA KIISLAMU

Written by on 20 October 2020

Polisi mjini Paris, Ufaransa imefanya misako iliyoilenga mitandao ya Waislamu wa itikadi kali baada ya tukio la kuchinjwa kwa mwalimu mmoja wa somo la historia siku tatu zilizopita. Mwalimu huyo alichinjwa baada ya kuwaonyesha wanafunzi wake kibonzo cha Mtume Muhammad. Mauaji yake yamezua hasira nchini Ufaransa na hapo Jumapili mamia kwa maelfu ya watu walishiriki […]

Read More

Load more